30 Jun 2020

Human trafficking / Utumwa mpya: wafanyikazi wa Kenya katika Mashariki ya Kati

Kenya bado haina sera ya ajira ya kigeni inayosimamia usafirishaji wa wafanyikazi.

Mnamo Septemba 2014, Kenya ilipiga marufuku usafirishaji nje wa wafanyikazi hadi Mashariki ya Kati kwa sababu wafanyikazi walikuwa wakisafirishwa kwa njia haramu na mitandao ya jinai iliyowapa kazi. Muhtasari huu wa sera unawalenga wahalifu ambao wanaendesha soko hili na unachunguza juhudi za serikali na wadau wengine za kuharamisha desturi hiyo. Ingawa hatua zilizopo zinastahili kupongezwa, hazitoshi. Upungufu mwingi bado unawawezesha wahalifu kuendelea kufanya kazi katika soko lenye faida, linalodhibitiwa kwa kiwango kidogo. Utafiti wa nyanjani uliofanywa umebaini kuwa biashara haramu ya binadamu bado ipo nchini Kenya.

Kumhusu mwandishi

Mohamed Daghar ni mtafiti katika mpango wa ENACT ulioko Nairobi. Hapo awali alifanya kazi na serikali na vituo vingine vya utafiti akichanganua maeneo ya uhalifu yanayobadilika na namna ya kukabiliana nayo. Ana Shahada ya Uzamili katika masomo ya amani, migogoro na maendeleo kutoka Universitat Jaume I, Uhispania. 

Photo © Adobe Stock

Related

More +

EU Flag
ENACT is funded by the European Union
ISS Donors
Interpol
Global
ENACT is implemented by the Institute for Security Studies in partnership with
INTERPOL and the Global Initiative against Transnational Organized Crime.