Masuala ya uongozi duni yameiweka Bandari ya Mombasa katika msururu mkubwa wa uhalifu ambao umepangwa unaovuka mipaka. Katika mwongo mmoja uliopita, Bandari ya Mombasa inayopatikana mashariki ya pwani ya Afrika imekuwa ikifanyiwa upanuzi na kugeuzwa kuwa ya kisasa, huku mabadiliko haya yakilenga kuboresha utendakazi wake. Lakini udhalilishaji unaofanywa na wanasiasa wanaowajua watu maarufu unaolenga kushawishi maamuzi muhimu ya usimamizi mkuu katika bandari hii inayomilikiwa na serikali umetatiza mabadiliko na kuiwacha bandari hii katika hatari ya kuathiriwa na mitandao ya uhalifu inayotekeleza shughuli zake bila woga.
Kumhusu mwandishi
Deo Gumba, Mratibu wa Uchunguzi wa Uhalifu ambao Umepangwa wa Afrika Mashariki wa ENACT, amefanya utafiti wa sera na kuchapisha masuala mengi yanayohusiana na usalama na uhalifu ambao umepangwa unaovuka mipaka.
Picha ya Jalada © Adobe Stock – Kalyakan.