Biashara haramu ya misandali nchini Kenya ni biashara ya mamilioni ya dola ambayo inanyonya jamii za wenyeji na kusababisha uharibifu wa misitu. Biashara haramu ya misandali imedumishwa na mtandao wa wahusika, kuanzia ngazi ya jamii hadi masoko ya kimataifa. Hili limesababisha uharibifu wa misitu ya jamii na imeweka mti wa misandali katika hatari ya kutoweka. Huku hayo yakitendeka, wahusika wa ngazi ya kati na ya juu katika mtandao huu wa uhalifu wanaendelea kujitajirisha.
Ingawa mamlaka ya kulinda misandali iliyo porini ni ya Huduma za Misitu ya Kenya, udhaifu katika Sheria ya Uhifadhi na Usimamizi wa Misitu Namba 34 ya mwaka 2016 umewezesha kufunguliwa mashtaka kwa kesi za biashara haramu ya misandali kupitia Sheria ya Uhifadhi na Usimamizi wa Wanyamapori ya 2013. Mkanganyiko ambao umetokana na ukosefu wa uwazi juu ya nani ana mamlaka ya utekelezaji umewapa ujasiri wafanyabiashara haramu wa misandali wanapowasilishwa mahakamani. Zaidi ya hayo, kukosekana kwa uwiano katika sheria za uhifadhi za Afrika Mashariki kumewezesha zaidi ulinzi wa misandali ya Kenya inayosafirishwa kimagendo hadi Uganda na Tanzania.
Kumhusu mwandishi
Dkt Willis Okumu ni mtafiti mwandamizi katika ISS kwenye Mpango wa ENACT, na yuko Nairobi. Hapo awali alifanya kazi kama mratibu/mtafiti wa ujenzi wa amani katika Huduma za Maendeleo ya Kianglikana Kenya. Maeneo yake ya utafiti ni pamoja na uhalifu wa kimataifa uliopangwa, uhusiano wa binadamu na mazingira, ujenzi wa amani baina ya jamii na maisha ya wafugaji katika Afrika Mashariki na Pembe ya Afrika. Ana shahada ya Uzamifu katika anthropolojia ya kijamii, Uzamili katika utamaduni na mazingira barani Afrika kutoka Chuo Kikuu cha Cologne, na Shahada katika sayansi ya siasa na sosholojia kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi.